Shule ya Sekondari Tusiime inawatangazia nafasi za kujiunga kidato cha kwanza 2020
Fomu za kujiunga zinapatikana
Tusiime Secondary school-DSM | – | Simu: 0652227792, 0754421215, 0713371231, 0784919670 |
Msimbazi Centre chumba namba 9 na 19-DSM | – | Simu: 0689 973 848/0689 384 819 |
Ms. Rose Precision Air Office (Bukoba) | – | Simu: 0787616806, 0765017601 |
Ms, Mariana Mothers Traver Agency Airport (Mwanza) | – | Simu: 0785874558, 0655672404 |
Au Pakua Fomu za Kujiunga Hapa |
Gharama ya Fomu ya maombi (Application Form) ni Shilingi 30,000/=
UTARATIBU WA KUJIUNGA
Hatua 1
Kujaza Fomu
- Jaza Fomu ya Udahili;- Majina ya mwanafunzi yatakayojazwa kwenye fomu ni lazima yaendane na yale yaliyomo kwenye cheti chake cha kuzaliwa
- Ambatanisha picha mbili za rangi (Passport Size) pamoja na kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
Hatua 2
Rejesha Fomu
- Pata risiti toka shuleni au msimbazi, au sehemu ulipochukulia fomu. Kama ni kwenye mtandao utakaporudisha fomu shuleni utapewa risiti.
- Rejesha fomu iliyojazwa shuleni mara tu baada ya kujaza ili kujihakikishia nafasi
Hatua 3
Mtihani wa udahili
Mwanafunzi atatakiwa kufanya Mtihani wa kuandika kwa masomo (04) ambayo ni; Hisabati, Lugha (Kiswahili na Kingereza) Maarifa ya Jamii na Sayansi.
- Mtihani wa kwanza utafanyika tarehe 16/09/2019 siku ya Jumatatu saa 01:30 asubuhi – 08:00 mchana hapa shuleni.
- Mtihani wa pili utafanyika tarehe 23/09/2019 siku ya Jumatatu saa 01:30 asubuhi – 08:00 mchana.
- Mtihani wa tatu utafanyika tarehe 30/09/2019 siku ya Jumatatu saa 01:30 asubuhi – 08:00 mchana.
Hatua 4
Matokeo
- Matokeo ya mtihani yatatoka mara tu baada ya mtihani.
- Kuchukua matokeo ya Mtihani na mapendekezo ya Bodi ya usaili muone mkuu wa shule au ofisi ya Wahasibu.
Zingatia
- Kutakuwa na Mafunzo ya awali ya kujiandaa na Kidato cha kwanza (Pre –Form One Course) yatakayogharamiwa na mzazi. Mafunzo haya ni muhimu sana kwa ajili ya kumjengea mwanafunzi msingi imara wa kujiandaa kuanza kidato cha kwanza.
- Kwa wale wanafunzi watakaoonekana kufanya vibaya katika mtihani wa usaili, watatakiwa kujiunga na mafunzo haya ya awali kwa lengo la kupata nafasi ya kujiunga na shule yetu.
- Hata hivyo, kutokana na umuhimu wa mafunzo haya ya maandalizi kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza, vilevile mwanafunzi atakayefanya vizuri mzazi unashauriwa mwanao asome masomo haya ya maandalizi ili kuzidi kumjengea msingi imara badala ya kumuacha akae nyumbani.
- Masomo haya yataanza tarehe 23/09/2020.
- Nafasi zipo za kutwa na bweni. Wanafunzi wa bweni watatakiwa kuripoti 20/09/2019 kuanzia saa 2.00 asubuhi na wanafunzi wa kutwa watatakiwa kuripoti tarehe 23/09/2019 saa 1:30 asubuhi.
- Muda wa mafunzo haya ni miezi mitatu ( Kuanzia tarehe 20/09/2019 – 20/12/2019).